Mazungumzo ya amani ya Sudan kusini yanatarajiwa kuanza mjini Addis Ababa Ethiopia wakati Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar wakitarajiwa kukutana siku ya Jumanne.Huu ni mkutano wa kwanza kati ya wanasiasa hao tangu watie saini makubaliano ya kusitisha amani mnamo mei 9.
Mkutano huu unajiri wakati ambapo hakuna maafikiano ya kumaliza vita nchini Sudan kusini vilivyoshuhudiwa kwa takriban miezi sita sasa.
Licha ya viongozi hao wawili kukubali kufanya kazi pamoja, wawakilishi wao wamekuwa wakitoa taarifa za kulaumiana katika mikutano iliyofanyika katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.Huu ni mkutano wa kwanza kati ya wanasiasa hao tangu watie saini makubaliano ya kusitisha amani mnamo mei 9.

Mkutano huu unajiri wakati ambapo hakuna maafikiano ya kumaliza vita nchini Sudan kusini vilivyoshuhudiwa kwa takriban miezi sita sasa.
Licha ya viongozi hao wawili kukubali kufanya kazi pamoja, wawakilishi wao wamekuwa wakitoa taarifa za kulaumiana katika mikutano iliyofanyika katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Lawama kutoka pande zote
Kila upande ukimshutumu mwenzake. Kundi la Machar linaliliaumu kundi la rais Salva Kii kwa kushindwa kuiongoza nchi na linamtaka kiongozi wa taifa hilo changa ajiuzulu.
Kwa upande mwingine, wafuasi wa rais Kiir wanasisitiza kuwa iwapo kutakuwa na mazungumzo yoyote ya kuunda serikali ya muungano, hawatomruhusu Machar awe kiogozi wa Sudan Kusini.
Umoja wa mataifa na Marekani zimetishia kuidhinisha vikwazo dhidi ya watu wa Sudan kusini iwapo hakutofikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi.
Makabiliano hayo yamesababisha vifo vya watu wengi na kusababisha zaidi ya watu milioni moja kukosa makaazi.
Mapigano yalianza Juba na kuenea katika maeneo mengine yakiwemo Bor, Jonglei na Bentiu.
Mkutano wa baraza la mawaziri wa shirika la IGAD utautangulia mkutano kati ya viongozi hao wawili.