Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya bure kwa waandishi wa habari kwenye maeneo matano, sekta ya uchimbaji, unyanyasaji wa kjinsia, kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya Kulevya kwa waandishi wa habari na utayarishaji na utengenezaji wa vipindi vya luninga na wanawake watangazaji jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma. kushoto kwake ni Msaidizi wa Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu, Dorothy Temu –Usiri na Mkurugenzi wa Mfuko wa vyombo vya habari, Ernest Sungura.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
WAANDISHI WA HABARI nchini wamehimizwa kushirikiana kwa karibu na Mfuko wa Vyombo vya Habari (TMF) ili kuacha kutegemea zaidi matangazo kwa sababu kuna weka taaluma yao rehani.
Akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari jinsi ya kuripoti mambo ya sekta ya uchimbaji, unyanyasaji wa kijinsia, kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya Kulevya na watayarishaji wa vipindi vya luninga, Waziri wa kazi na Ajira, Mhe, Gaudensia Kabaka amesema kwamba vyombo vya habari lazima vishirikiane na mfuko huo ili kuwa huru wakati wa kuripoti.
“kuendelea kutengemea matangazo kutoka kwenye makampuni mbalimbali ili kujiendesha kuna wafanya kutokuwa huru katika uandishi wetu na tasnia ya habari kwa ujumla,” amesema Kabaka
Amesema mradi huo wa mafunzo ya bure kwa waandishi ni muhimu kwa taifa kwa sababu tatizo kubwa la ajira hasa kwa vijana na wanawake linachangia kwa kiasi kikubwa vijana wengi kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
Baadhi ya wadau na wageni waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi hayupo pichani.
Kabaka aliongeza kuwa mafunzo haya yatakayotolewa kwa ufadhili wa TMF ni muhimu ili kuelimisha jamii madhara ya kuuza na kusambaza dawa za kulevya na matumizi yake yanavyoathiri kizazi na kizazi.
“kwa sasa nchi yetu ya Tanzania ni moja ya nchi zilizoathirika sana na matumizi ya dawa za kulevya na mbaya zaidi kutumika katika njia ya kusambaza madawa hayo hatari,”
“kwa mujibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii tuna jumla ya watu 20,626 walioathirika na dawa za kulevya na kwa sasa wanapatiwa matibabu,” alisisitiza Kabaka.
Amesema nchini matumizi ya dawa za kulevya kwa zaidi ni Bangi, Heroin, Mirungi na Cocaine na cha kutisha matumizi haya yanaathiri pia wanafunzi wa sekondari na shule za msingi nchini.
Msaidizi wa Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu(UNFPA), Dorothy Temu Usiri akitoa nasaha zake kwenye uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
Kwa upande wake, Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu, Dorothy Temu-Usiri amesema kuwa kuongezeka kwa vitendo vya kikatili vya kijinsia na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi vimechochea kushirikiana na TMF kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari hapa nchini.
“kwa kuanzisha mafunzo haya ya bure kutasaidia waandishi wa habari kuandika kwa kina juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ambazo ndio kichocheo cha ukatili wa kijinsia hasa kwa Wanawake,” amesema Usiri
Usiri aliongeza kwamba nchini Tanzania idadi kubwa ya watu wenye nguvu ya kufanya kazi ni vijana kwahiyo ni muhimu jamii ya kimataifa kushirikiana na serikali na taasisi zingine ili kunusuru kundi hili muhimu kwenye nchi.
Mkurugenzi wa TMF nchini, Ernest Sungura akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa mafunzo ya bure yanayofadhiliwa na mfuko wake ambapo amesema kwamba malipo madogo kwa wahariri na waandishi wa habari kunadidimiza taaluma ya uandishi wa habari pamoja na swala la kutokubobea katika sekta husika (Specialization).
Wadau watakaoshiriki kwa ukaribu kwenye mradi huo wakitambulishwa kwa mgeni rasmi kutoka kushoto ni Dkt. Pilly Said kutoka kitengo cha madawa ya kulevya hospitali ya Mwananyamala, January Nzisi Mkuu wa Kitengo cha Mtandao Tume ya Kudhibiti Madawa ya kulevya, Geodfrey Nzowa, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, kitengo cha Kupambana na Madawa ya Kulevya, Bi. Aida Teshe Kaimu Kamishina kutoka Tume ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya (DCC) na Florence Bahati Khambi Afisa Habari kutoka Tume ya Kudhibiti dawa za kulevya.
Wadau mbalimbali na wageni waalikwa wakifuatilia yaliyojiri kwenye uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya bure kwa waandishi wa habari kwenye maeneo matano, viwanda, jinsia, madawa ya kulevya, kuzuia madawa ya kulevya kwa waandishi wa habari na utayarishaji na utengenezaji wa vipindi vya luninga na wanawake watangazaji jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
Afisa Habari kutoka kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari (UNIC), Stella Vuzo amesema kwamba mradi huo umekuja katika muda mwafaka kwa taifa la Tanzania kwa sababu takwimu za matumizi ya dawa za kulevya zinatisha kwa vijana ni lazima taasisi za ndani na jamii za kimataifa kushirikiana kupambana na janga hili.
Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo katika maeneo mbalimbali.
Afisa Habari kutoka kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari (UNIC), Stella Vuzo (kulia) pamoja na Bw. Phillip Musiba kutoka UNIC.
Afisa mafunzo wa TMF, Bi. Raziah Mwawanga akinakili mambo muhimu yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA(Mstaafu) Ananilea Nkya (kushoto) na Mwandishi wa Habari Mkongwe Mama Eda Sanga (katikati) ambaye ni miongoni mwa mentors kwenye mradi huo. Kulia Sawiche Wamunza kutoka UNFPA.Kwa matukio zaidi ingia humu
0 Comments