Viongozi wa Afrika Kusini wameadhimisha siku ya kimataifa ya kusherehekea maisha ya Mandela
Tarehe 18 julai ni siku ya kimataifa ya kusherehekea maisha ya hayati Nelson Mandela.
Wananchi wa Afrika Kusini wamekuwa wakifanya shughuli mbali mbali za kijamii kumkumbuka Moja ya shughuli hizo imekua kufanya usafi.
Waziri wa Mambo ya nchi za njee wa A-Kusini pamoja na kikosi cha mabalozi kadha wanaoishi A-Kusini wameweza kufanya usafi katika kituo kimoja cha magari ya abiria (Daladala) mjini Pretoria.
Huu ulikuwa wito wa Rais Jacob Zuma kwa raia wa afrika ya kusini kulisafisha taifa lao.
Lakini baadhi yao wamelalamika wakisema kuwa hiyo ni kazi ya serikali.Ili kuadhimisha kuzaliwa kwake mamilioni ya watu pia wamejitolea kutumia dakika 67 za mda wao kufanya mambo mema ili kuadhimisha miaka 67 aliyotumia kama mwanaharakati wa kisiasa.
Vuguvu hilo lilianzia mjini Johanesburg na New York mnamo mwaka 2009 lakini sasa linasimamia mataifa 126.
Bwana Mandela, aliyefariki mwaka jana alisifika sana kwa kupigana vita dhidi ya utawala wa mzungu.
Aliishi grezani mwa miaka 27 kabla ya kuwa rais wa kwanza mzalendo nchini Afrika Kusini mwaka 1994.
Kabla ya kifo chake aliugua homa ya mapafu kwa mda mrefu, ugonjwa ambao mara kwa mara ulikuwa unazuka mwilini mwaka hata baada ya matibabu.
Mnamo siku ya Alhamisi, vitu vinavyosimulia maisya yake vilinadiwa kama kumbukumbu kwa maisha yake na kuchangisha pesa ili kusaidia shirika la kibindamu.
|
0 Comments