Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akiwasili kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Na Mwandishi wetu
Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala, Jerry Silaa ameipongeza makampuni yaliyochini ya Kundi la METL kwa kuhakikisha ajira kwa watanzania na soko la mali ghafi kwa wakulima wa bidhaa mbalimbali nchini.
Silaa alisema hayo jana wakati alipotembelea banda la METL na kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na makampuni yake mbalimbali zikiwemo bidhaa za michikichi na katani.
Alisema kwa kutengeneza sabuni, mafuta na mali ghafi nyingine kutokana na michikichi kampuni za Metl zinawezesha wakulima kujiendeleza na pia kuwa na uhakika wa soko.
METL yenye makampuni zaidi ya 25 sehemu kubwa ya bidhaa zake zinatokana na mali ghafi inayozalishwa nchini na nyingine ni zile zinazotumika kwa ajili ya wakulima kama matrekta.
Aidha katika banda hilo kubwa ambapo kulijaa aina mbalimbali ya bidhaa kuanzia Sabuni,Vitenge, mafuta ya Mawese,vinywaji baridi, Matrekta na bidhaa za nyumbani, Mstahiki meya huyo alichezesha bahati nasibu za watu waliotembelea banda hilo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi za Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE kwenye viwanja vya maonesho ya Sabasaba mara baada ya kuwasili.
Akizungumzia uwekezaji wa METL, Silaa alisema kwamba anafarijika na jinsi bidhaa za kampuni hizo zinavyoimarika ubora kila mwaka na kusema wakati umefika kwa serikali kuangalia wawekezaji wazawa.
Alisema kwa maoni yake serikali ione jinsi ya kuwasaidia wawekezaji wanaoagiza mitambo toka nje ili kodi wanaoyotakiwa kulipa wailipe baada ya kuanza kazi za uzalishaji.
“Hii itasaidia sana kuwa na wawekezaji wa ndani ambao wataweza kutoa huduma kama soko la mali ghjafi na pia kuongeza thamani ya bidhaa zinazoalishwa kutoka Tanzania” alisema silaa.
Aidha Silaa alipongeza MeTL Group kwa kuweza kutoa ajira kwa watanzania wazawa huku bidhaa zake nyingi zikiwa kimbilio la watanzania wote, hasa wa kipato cha chini.
Afisa Mwandamizi wa TANTRADE, Fidelis Mugenye, (kushoto) akimuonyesha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa ratiba ya ziara kwenye mabanda mbalimbali ya maonesho ya Sabasaba yanayokaribia kufikia ukingoni.
“Naipongeza MeTL Group, kwa kuzalisha bidhaa bora ambazo ni kimbilio la wananchi wengi… hasa bidhaa zake za mafuta, sabuni, unga, vinywaji na bidhaa zingine kibao” alisema Silaa
Pia aliipongeza MeTL kwa upande wa kutoa ajira na kukuza uchumi hapa nchini, ikiwemo kuzalisha bidhaa nyingi na zenye ubora ikiwemo za kamba ya mkonge ambayo alisema ni majibu ya utunzaji wa mazingira kutokana na vifungashio vya plastiki kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira.
Katika bahati nasibu iliyochezeshwa mkazi wa Kijitonyama Jijiji Dar es Salaam, Irene Manamba amejishindia zawadi ya pikipiki mpya.
Aidha, katika droo hiyo, washindi wengine waliojishindia zawadi mbalimbali katika droo hiyo majina yao na wanakotoka ni Victoria Charles ambaye alikuwa mshindi wa pili mkazi wa Temeke, Julius Kamele (Tabata), Irene Mushi (Kijitonyama), Semi Anderson ((Dar es Salaam), Happyness Kalokola (Kitunda), Noel Kalenga (Sinza Kumekucha), Adam Mkwaya (Mabibo), Mery Msangi (Dar es Salaam) na Aisha Abeid (Tabata).
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa akisalimiana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa ndani ya ofisi za Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (katikati) akiongozwa na vijana wa skauti kuelekea kwenye mabanda mbalimbali huku akiwa ameambatana na msaidizi wake Anthony William (kushoto).
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (katikati) akipata maelezo ya sabuni mpya ya MO BEAUTY kutoka kwa Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Kelvin Msangi (kushoto) mara baada ya kuwasili katika banda hilo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali.
Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali akimuonyesha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaabaadhi za Vitenge na Khanga (hazipo pichani) vinavyozalishwa na kiwanda cha 21st CENTURY Textile Ltd chini ya MeTL GROUP alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (wa pili kushoto) akipewe maelezo ya ladha za aina tofauti za soda zinazotengenezwa na kampuni hiyo kutoka kwa Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Kelvin Msangi (wa pili kulia) kabla ya droo maalum kwa wateja wanaotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akipata maelezo ya sabuni mbali mbali za unga kutoka kwa Mfanyakazi wa Royal Soap Detergent Industries, Aneth Masesa alipotembelea banda la MeTL GROUP kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto) akipata maelezo ya aina tofauti za kamba na magunia yanayotengenezwa na kampuni hiyo kutoka kwa Mtaalamu wa Mkonge wa MeTL GROUP, Bw. Iddi Omari (wa kwanza kulia) wakati alipotembelea banda la MeTL GROUP kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw. Mrisho Millao (kushoto) akichanganya boksi lenye majina ya wateja waliotembelea Banda la kampuni ya MeTL GROUP na kujaza kuponi za kushiriki kwenye droo ya Bahati nasibu ambayo imechezeshwa jana kwenye Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (wa pili kulia), Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali (kulia) na Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group, Kelvin Msangi (wa pili kushoto) wakishuhudia tukio hilo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, akichagua kuponi ya mshindi wa kwanza kwenye droo kubwa ya Kampuni ya MeTL GROUP kwa wateja waliokuwa wanatembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali na Kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group, Kelvin Msangi.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (wa pili kulia) akimtangaza mshindi wa droo maalum kwa wateja wanaotembelea banda la MeTL GROUP kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.Na Mshindi huyo ameshinda Zawadi ya Pikipiki aina ya A1 ambayo imesajiliwa na seti mbili ya Vitenge,Wa kwanza kushoto ni msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahatinasibu Bwana Mrisho Millao.Wanaoshuhudia wa pili kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Kelvin Msangi na Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali (wa Kwanza kulia).
Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Kelvin Msangi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) namna washindi kumi waliopatikana watakavyochukua zawadi zao mara baada ya kupigiwa simu na wahusika kwa ajili ya kukabidhiwa zawadi hizo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (katikati) akipokea zawadi ya soda za MO Cola kutoka kwa Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali. Kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Kelvin Msangi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akiondoka kwenye banda la MeTL GROUP mara baada ya kumaliza shughuli ya kuchezesha droo ya bahati nasibu kwa wateja wanaotembelea banda la MeTL Group kwenye maonesho hayo.
Mtaalamu wa kutembea juu kamba nchini Hassan Mkenjula a.k.a SPIDERMAN akitoa burudani ya kupiga danadana kwa kutumia mdomo kwenye banda la MeTL GROUP.
0 Comments