Mlipuko mkubwa umetokea na milio ya risasi imeripotiwa karibu Bunge la Somalia wakati wabunge wakiwa katika kikao chao.
Habari za awali zinasema kuna watu kadhaa wamejeruhiwa kutokana na mlipuko huo unaosemekana umesababishwa na bomu lililolipuka kwenye gari.
Watu kumi walikufa wakati kundi la kiislamu la wapinganaji la Somalia Al Shabaab waliposhambulia jengo la bunge wiki sita zilizopita.
Kundi la Al shabaab lilipoteza udhibithi katika mji mkuu wa Mogadishu tangu mwaka 2011 na tangu wakati huo limekuwa likiendesha mashambulizi ya mabomu na kufanya mauaji.
Mapema wiki hii Mbunge maarufu Ahmed Mohamud Hayd, aliuawa kwa kupigwa risasi katika mji huo, katika shambulio linalodaiwa kufanywa na Al Shabaab.
|
0 Comments