Balozi Manongi akiwaombea marehemu
Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, akizungumza machache na Muwakilishi wa Kudumu wa Udachi katika Umoja wa Mataifa, Balozi Karel van Oosterom mara baada ya Balozi Manongi kusaini kitabu cha maombolezo.
"Asante sana kwa kuja kutufariji katika kipindi hiki kigumu, asante sana, natambua vema ushirikiano mzuri uliopo baina ya serikali zetu".
ndivyo aliyosikika akisema Muwakilishi wa Kudumu wa Udachi Balozi Karel van Oosterom
Mhe. Balozi Tuvako Manongi, Muwakilishi wa Kudumu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jana Jumatano ameungana na Mabalozi wengine wanaoziwakilishi Nchi zao katika Umoja wa Mataifa, kutia saini kitabu cha maombolezo kilichofunguliwa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Udachi ( Netherlandes) katika Umoja wa Mataifa kuwakumbuka watu 298 waliopoteza maisha baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria ya MH17 inayomilikiwa la Shirika la Ndege la Malaysia kuangushwa katika eneo la Mashariki ya Ukraine wiki iliyopita. Idadi kubwa ya abiria hao walikuwa ni raia wa Udachi.
0 Comments