Mfungaji wa goli la Ujerumani Hummels akifunga bao kwa njia ya kichwa na kuipeleka Ujerumani robo fainali.

Ujerumani Imesajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ufaransa katika mechi ya robo fainali.

Kufuatia ushindi huo dhidi ya Ufaransa ndiyo timu ya kwanza kuwahi kufuzu kwa nusu fainali katika mashindano manne ya kombe la dunia mfululizo .Ujerumani ndiyo timu ya kwanza kufuzu kwa nusu fainali ya kombe la dunia huko Brazil.
Kufuatia ushindi huo Ujerumani watakutana na mshindi baina ya Brazil na Colombia katika hatua ya nusu fainali .