INAWEZEKANA lisiwe jibu sahihi lakini kwa kiasi fulani linatoa picha juu ya kinachoendelea kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva, kila kona gumzo ni juu ya nani mkali kimuziki kati ya Diamond Platnumz dhidi ya Ali Kiba.Nasibu Abdul ‘Diamond’ ndiye staa kwa sasa na amedumu kileleni kwa miaka kadhaa, hilo halina ubishi, lakini Ali Kiba amerejea kwa kutoa nyimbo mbili za Kimasomaso na Mwana baada ya ukimya wa miaka kadhaa, ukijumlisha vijembe ambavyo wanapigana wawili hao kwenye vyombo vya habari, gumzo limekuwa kubwa juu ya nani ni mkali kati yao kimuziki.Ali Kiba ambaye anatarajiwa kufanya shoo yake ya kwanza kubwa tangu aliporejea, katika Tamasha la Matumaini kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Agosti 8, 2014, ameonekana kuongoza kwenye kura za maoni juu ya nani mkali kati yake na Diamond kupitia kuraza za mitandao ya kijamii zikiwemo Twitter na Facebook.
Diamond Platnumz
Alipoanza kusika wengi waliamini angepotea kama ilivyotokea kwa wengi, lakini amedumu na kuwa msanii mkubwa, kazi zake na wasanii wa nje zimemuongezea thamani na ameonekana kuwa mwenye thamani kubwa zaidi kuliko wengine katika Bongo Fleva. Anastahili pongezi kwa kuendelea kubaki kileleni kwa miaka zaidi ya mitatu.


Ali Kiba

Sauti yake ndiyo silaha kubwa, alikuwa msanii mkubwa kiasi cha kuimba wimbo mmoja na R. Kelly ambaye naye alikiri kushangazwa na uzuri wa sauti ya kipekee ya Kiba. Hakutoa wimbo kwa miaka mitatu lakini bado hakujishusha thamani kila alipotakiwa kwenye shoo, amerejea, anadai kiti chake hakikuwa na mtu, ila kilikuwa na vumbi, sasa anakipangusa na kukaa mwenyewe.

Maoni ya mashabiki:
Ubora wa msanii mara nyingi unabaki kwa shabiki mwenyewe kutokana na kile ambacho anahitaji kukisikiliza au kukiona, kura zilizopigwa kupitia facebook.com/championi.newspaper na twitter.com/ChampioniNews zimeonyesha Ali Kiba anakubalika zaidi kama ifuatavyo:
Hoja ilikuwa hivi: Unadhani nani mkali kwenye tasnia ya muziki kati ya Ali Kiba Vs Diamond...
Jackson Masawe: Diamond
Gabrinho Joel: Naona kama umeniuliza Cr7 na Messi. Hapo ni kipaji Vs nyota, Ali Kiba anatisha.
Hans Mloli: Ali Kiba 4 Real.
Emmanuel Lukamisa: Ali Kiba.
Ezeki Dimoso: Ali Kiba anajua tafuta kitu kingine cha kuweka.
Ismail Honde:  Ali Kiba.
Cretus Cray: Ali Kiba weka mbali na watoto, huyo mwingine ni zali tu ila hana kipaji chochote.
Nancy R Da Silva: Kiba 4 real.
Bon Jos Makanza: Ali Kiba ana kipaji cha muziki, Diamond kakurupuka kama mnabisha hesabuni miaka minne mbele,
Did Abdallah Mchoo: Ali Kiba.
Felyx Mwashala: Ali Kiba nouma wewe. Mapenzi yana-run dunia.
Faustine Zephania Nyakarungu: Ali Kiba habari ya mjini.
Twahir Mohamedi: Ali Kiba habari nyingineeee.
Neema Rupia: Diamond.
Mlambo Lukwaro: Diamond yuko juu.
Isihaka Kaburu: Wote wakali.
Amir Maftah: Kiba anakaba hadi penalti, hebu muulize R.Kelly kuhusu hilo.
Petro Ngole: Diamond mkali nyie, tatizo huyu jamaa anavaa nguo za kubana mapaja.
Ally Hadi: Ali Kiba.

Sadam A Kilapo: Diamond!
Mahamoud Shilah: Ali Kiba mkali kimuziki ila anazidiwa kitu kimoja tu, ukubwa wa d***.
Ally Said: Ali Kiba ndiyo habari ya mjini.
Kidy  Zilla: Ali Kiba.
Said Maeda: Kiba anampoteza mbaya Diamond.
Peter Java: Ali Kiba mashine nyingine hiyo, siyo muuza sura, kwake ni kazi tu.
Flora Cosmas: Tangu nimjue Ali Kiba hajawahi kukosea. Kila nyimbo anayotoa inakuwa kali zaidi ya ile ya awali, Kiba 4 real ndiyo mpango mzima.
Okelo Komba: Ali Kiba ndiyo habari ya mjini.
Michel Masawe: Diamond ni mashine.
Yohana Samwel: Ali Kiba ndiyo mpango mzima.
Marks Man Mganga: Diamond ndiyo mpango, wasafiii.
Costar Ngoila: Diamond ni shida.
Shaaban J. Fernandinho: Diamond.
Stephen Luoga: Wote wakali sana ila kila mtu ana muda wake.
Abuu Rick Binboy: Diamond.
Sylvester Mathias: Ali Kiba.
Jerome Makwinya: Diamond Platnumz.

Docker Amiri: Ali Kiba.
Farouk Ismail: Kiba 4 real…Yuko juu.
Delila Mdachi: Ali Kiba.
Wazily Mbunda: Platnumz ndo mpango
Michael Julius: Ali Kiba.
Johari Elasto: Wote wako vizuri.
Zayatte Cheonsa Michael: Kwa sasa Diamond yupo juu sana.
Tusah Samwel: Ali Kiba.
Anicet Octavian: Kiba 4 real.
Lydia Joseph: Ali Kiba.
Tinno Josse: Ali Kiba 4 sure anatisha.
Bildady Paul: Ali Kiba.
Sam Black: Ali Kiba juuuu!
Willy Leonard: Ali Kiba chapa nyingine.
Jasmine Idrisa: Ali Kiba.
Mick Songo: Ali Kiba.
Makaveli Mshua: Ali Kiba.

Samweli Gimase: Kiba for real kwa kuwa hachuji, chipukizi Diamond ameimba na hizo nyimbo kasaidiwa tu na Bob Junior.
Magere Michael: Ali Kiba yupo juu mpaka kesho.
Mishi Zanuzaj: Ali Kiba yupo juu hawamuwezi.
Nyamaty Anyireal: Kumchukia mtu kisiwe chanzo cha kumnyima haki yake, Diamond anajitahidi.
Thomas Chessam Montana: Ali Kiba.
Habibu Duka: Ali Kiba ndio habari ya mjini.
Bosko Geradde: Ali Kiba.
Ramadhani: Ali Kiba.
Majeshi Elias: Ali Kiba.
 Salma Omary: Ali Kiba.
Rhobi Moremi: Diamond mpango mzima.
Ally Ramadhan: Ali Kiba.
Leokadia Shayo: Ali Kiba.
Ngassa Emmanuel: Wote wakali kila mmoja anakubalika kivyake.
Charlie Lintu: Ali Kiba.
Killo John: Ali Kiba ndiyo mkali Bongo.
Christina Charles: Diamond ni mpango mzima.
Pius Biraro: Diamond anatisha.
Juma Madee: Kitaa ndiyo kinajua Ali Kiba ni nani. Kiba ni sheeeda! Diamond ni msanii, Kiba ni mwanamuziki.
David Mlaponi: Ha ha ha! Aliyeanza kaanza, Kiba habari nyingine.
Reuben Kanju: Diamond.
Ambrose Joseph Butilaga: Ali Kiba.
Jamila Daudi: Diamond.
Hamza Komanya: Kiba 4 life.
Johari Mawazo: Ali Kiba yupo juu.
Dismas Seleman: Ali Kiba.
Sharifa Juma Hamis: Wote nawakubali lakini Diamond ni noma sana.
Rigobert Maro: Ali Kiba.
Said Rashid: Ali Kiba.
Husseni Khalid Malende: Ali Kiba.
Gustafu Justine: Ali Kiba anatisha.
Almas Kibehere: Ali Kiba ni balaa.
Abed Wa Kwanza: Ali Kiba.
Nicolaus Trac: Diamond ni noma, Kiba ilikua zamani.
Kagawa Kp: Acheni kuwashindanisha densa na msanii. Kiba yuko juu.
Eric Madaha: Ali Kiba.
Joseph Nkondo: Ali Kiba zaidi.
Said John Seiph: Ali Kiba.
Johari Mawazo: Ali Kiba.
Nadia Said: Ali Kiba kiboko yao.
Athuman Chiepo: Ali Kiba.
Rigene Mbalula: Diamond mkali sana.
Gaston Sebastian: Platnumz.
Sammyto Malekani: Diamond mkali zaidi.
Haji Fuko: Diamond kwa kuwa anauza zaidi.
Baba Corine: Diamond ni noma, Kiba ilikua zamani.
Karume Malembeka: Ali Kiba mkali ila hana nyota.
Johari Ally: Platinum anatisha.
Ally Ibrahim: Ali Kiba.
Festo JM: Kiba noma.
Ally Ibrahim: Uko juu sana ndugu yangu Ali Kiba.
Isack Melkzedek: Kiba bado sana na ataendelea kusubiri. Diamond ni moto mwingine
Saadat Omary: Ali Kiba.
Isihaka Hassan: Ali Kiba bana.
Jofrey Mwaluswaswa: Kiba mzuri ila Diamond ni maarufu.
Clarence Mulisa: Diamond anatisha.
Felix Msuva: Ali Kina ndiyo kila kitu.
Kabaly Faraji: Ali Kiba.
Faraji Mahyadi: Ali Kiba.
Styne De Charz Celestinho: Ali Kiba nouma.
Fadhili Athumani: Ali Kiba.
Hassan Mohamedi: Ali Kiba hatari sana siyo huyo mwizi wa nyimbo.
Perfume Boy Raheem: Kiba anatisha.
Immanuel Sylous: Ali Kiba watakaa sana,
Mwarami Juma: Ally Kiba 4real.
Samwel Mafuwe: Ally Kiba mashine nyingine!
Julius Matee: Kiba noma.
Hafidh Mbaruku: Ali Kiba 4 real.
Said Uladi Ally Nachoma: Diamond yuko anga za kimataifa.
Bahath Batiso: Hatuangalii muziki wa waganga tunataka kipaji. Ali Kiba ni nouma sana.
Isihaka Kaburu: Mkali Diamond Platnumz.
Ben Bugalama Pasabu: Mimi namkubali Ali Kiba.
Mohamed Mashango: Unafananisha panga na AK47 au kujipa zambi za bure, Diamond mkali.
Isack Melkzedek: Platinum yuko juu sana tena sana.
Abubakari Said: Kiba historia nyingine.
Stephano Komba: Diamond yupo juu.
Mussa Kisamo: Hao jamaa Level zao zinalingana.
Juma Omary: Diamond.
Boniphace Robinson: Diamond anatisha yupo anga ya kimataifa.
Hassan Omary Kirukuu: Diamond yupo sawa.
Hassan Kingo: Ali Kiba mtu mwingine.
Mhamila Rajabu: Ali Kiba juu hakuna ubishi.
Tinophil Chamkae: Tuache ushabiki kwa sasa Diamond yupo juu.
Bahath Batiso: Diamond nampa kura yangu.
Baraka Juma: Ali Kiba.
Kazumba Waissa: Ali Kiba yuko sawa.
Hassani Amani: Ali Kiba
Felix Matingo: Ali Kiba ni nouma.
AB Chimasa: Ali Kiba noma sana.
Dominik Mibazi: Ali Kiba.
Martha Mkunde: Ali Kiba hakamatiki.
Innocent Pius: Ali Kiba mkali.
Maulid Dege: Diamond ni nouma.
Ndiefu Master: Kiba nooumaa.
Mwajeck Mtata: 100% Kiba.