Stori: Gladness Mallya
MKURUGENZI wa bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Ally Choki amesema yupo tayari kumaliza tofauti zake na bosi wake wa zamani anayemiliki kundi la African Stars, Asha Baraka.“Mimi niko tayari kuyamaliza na Asha Baraka, Global Publishers mlishajaribu kutukutanisha lakini sijui ilikuwaje, lakini kutokana na maneno ya busara mliyonipa, nitamsamehe endapo tutakutanishwa maana bifu hazimsaidii mtu yeyote,” alisema.Choki ambaye alijipatia umaarufu mkubwa alipokuwa kiongozi na mwimbaji nyota wa bendi hiyo maarufu kama Twanga Pepeta, ameshawahi kutofautiana mara kadhaa na mkurugenzi huyo anayejulikana kama Iron Lady, lakini pia wamekuwa wakipatana baada ya muda.
Hivi sasa wapo katika bifu kubwa kufuatia Choki naye kumiliki bendi inayopata mafanikio makubwa kiasi cha kuanza kunyang’anyana wasanii.
|
0 Comments