Habari zilizotufikia punde  chumba chetu cha habari ni kwamba Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam umeteketea kwa moto usiku wa leo. akiripoti toka eneo la tukio mwandishi wetu Rahim ambaye ametutumia picha hii anasema gari za zima moto zilikuwepo eneo la tukio lakini hali ya uzimaji ilikuwa ngumu kutokana na moto kuwa mkubwa eneo la ghorofa la mskiti huo.chanzo cha moto huo tutawaletea pindi habari kamili zikiwasili mitamboni.Maganga One Blog inatoa pole kwa waumini wote wa msikitini hapo kwa janga kubwa la moto lililosababisha maafa ya msikiti huo.
(Picha na Rahim wa Maganga One Blog Dar es Salaam)