Majeshi ya Israel imeanza tena upya operesheni yake ya mashambuzi katika eneo la Gaza baada ya kumalizika kwa saa 7 za kusitisha mapigano lililotolewa na na Israel kwa ajili ya huduma za kibinadamu katika baadhi ya mipaka ya Israel.
Waziri Mkuu wa Palestina Benjamini Netanyau amesema operesheni hiyo itaendelea hadi hapo hali ya usalama na utulivu utakaporejea nchini Israel.
Japokuwa kumekuwa na kupungua kwa kiwango cha mashambulizi nyakati za mchana, Wapalestina wameilaumu Israel kwa kuikuka walichokipanga wenyewe cha usitishaji wa mapingano na badala yake ikashambulia kwa bomu kambi ya wakimbizi katika eneo la kaskazini mwa Gaza na kuua mwanamke mmoja na mtoto wa miaka nane.
Israel imesema kwamba wapiganaji wa kiislamu wameendeleza upigaji wa mabumu katika ardhi ya Israel.
Katika mji wa Jerusalemu, Israel mwisreel mmoja aliuawa wakati trekta ya kuchimba mchanga ilipogonga basi jambo ambalo Israel imesma ni shambulio la kigaidi.
|
0 Comments