Majeshi ya Israeli yakijiandaa kwa mashambulizi ya ardhini dhidi ya Wapalestina
Waziri mkuu wa Isareli Benjamin Netanyahu ameonya kuwa taifa hilo halitasita kuishambulia Gaza hata baada ya operesheni inayoendelea ya kuharibu njia za chini kwa chini kukamilika.
Bwana Netanyahu alionya kundi la Hamas kuwa serikali yake itaiadhibu vikali kundi hilo iwapo itathubutu tena kuidhuru taifa hilo la Kiyahudi.
Matamshi hayo yanawadia huku kukiwa na hofu huenda mazungumzo ya kusitisha mapigano yanayoendelea huko Misri yakagonga mwamba.Zaidi ya wapalestina 1,655 na waisraeli 65 wamepoteza maisha yao tangu mapigano hayo yaanze yapata majuma matatu yaliyopita .