Stori: Musa Mateja
UZINDUZI wa Serengeti Fiesta 2014 juzikati ulirindima baada ya msanii wa kizazi kipya anayefanya poa kwa sasa Estelina Sanga ‘Linah’, kufanya balaa wakati wakiimba wimbo walioshirikiana na mkali Nasib Abdul ‘Diamond’ jukwaani.Wakati wawili hao wakiteka hisia za mashabiki kutokana na jinsi walivyokamua huku wakicheza shoo, pia wasanii mbalimbali nao walifanya vitu vyao jukwaani hapo, wachanga kwa wakongwe wakiwemo Young Killer na Mo music waliokuwa wenyeji.Wengine waliopata fursa ya kufanya makamuzi ya nguvu ni pamoja na Yamoto Bendi, Sky Light, Makomandoo, Chege na Temba, Madee, Nay wa Mitego, Stamina, Young Dee, Mr Blue, Nyandu Toz, Khadija Maumivu, Vanesa Mdee na baadaye Dogo Janja aliyepanda jukwaani ikiwa ni siku chache baada ya kutimiza umri wa miaka 18.