Mkurugenzi wa jiji la LAHTI, Kari Porra akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa 
nyumba hizo za mbao kwa mratibu wa ziara hiyo Godfrey Nyamrunda kutoka
taasisi ya Uongozi ya Tanzania, nyuma yao ni Meya wa jiji la Dar Esa
Salaam Dk Didas Masaburi.

Baadhi ya viongozi kutoka majiji sita ya Tanzania wakipata maelezo kuhusu mfumo wa ukusanyaji wa taka na uchujaji wa maji machafu katika jiji la LAHTI, kutoka kushoto ni mratibu wa mtandao wa majiji Tanzania, ( Tanzania Cities Network) Philoteus Mbogoro, Meya wa jiji la Tanga Omary Guledi, Lissa Tervo wa taasisi ya Uongozi ya Tanzania, Johanna Palamoki ambae ni mtaalam wa mipangomiji katika jiji la LAHTI, Mkurugenzi wajiji la Lahti Kari Porra na Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga ( picha zote na Vedasto Msungu wa ITV)
Badhi ya nyumba za ghorofa zilizojengwa kutumia mbao katika jiji la
LAHTI nchini Finland ambazo zilitembelewa na madiwani wa majiji sita ya
Tanzania waliokuwa katika ziara ya mafunzo nchini humo iliyoratibiwa na
taasisi ya Uongozi ya Tanzania. Finland ni miongoni mwa nchi zenye maeneo makubwa ya misitu ya
kupandwa dunaini, zaidi ya asilimia 80 ya eneo la nchi hiyo ni misitu
na wenyewe wanasema nyumba zinazojengwa kwa kutumia mbao zina gharama
nafuu kuliko kujenga kwa matofali au mawe.