TIMU ya Taifa ya Tanzania, 'Taifa Stars' imeondolewa katika kinyang'anyiro cha kuwania kufuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika 2015 baada ya kufungwa mabao 2-1 na timu ya Taifa ya Msumbiji 'Mambaz' leo.
Mechi hiyo imepigwa mjini Maputo nchini Msumbiji ambapo Stars imeondolewa kwa jumla ya mabao 4-3 baada ya sare ya 2-2 katika mchezo kwa kwanza uliopigwa jijini Dar Julai 20 mwaka huu.