Tukio hilo lililonaswa na gazeti hili lilifanyika kwa siku tatu mfululizo mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli maarufu iliyopo Posta jijini Dar wakitaka serikali ya Tanzania itambue na kuhalalisha mapenzi hayo ya jinsi moja na ikiwezekana hata katiba mpya inayotaka kuundwa sasa hivi viingizwe vipengele vinavyowahusu wao.Bila kujua anazungumza na mwanahabari wetu, mmoja wao alipoulizwa nini kinaendelea hotelini hapo, alisema mkutano huo unawahusu mashoga na wasagaji huku akibainisha kwamba unafanywa kwa siri kubwa.Baada ya kupata taarifa hizo, kachero wa Ijumaa Wikienda alizama ndani kimafia ambapo alinasa mazungumzo ya kikao hicho, ajenda kubwa ikiwa ni kuishinikiza serikali itambue uwepo wao hapa nchini. Ili kujua kama wizara inajua kinachoendelea, gazeti hili lilimtafuta Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba lakini simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea. |
0 Comments