Maafisa wa polisi nchini Pakistan wamekabiliana na waandamanaji wanaopinga serikali wanaoelekea katika makao rasmi ya waziri mkuu Nawaz Sharrif katika mji mkuu wa Islamabad.
Mmoja ya viongozi wa maandamano hayo Tahir Ul-Qadri amesema kuwa maafisa wa polisi waliwafyatulia risasi pamoja na kuwarushia vitoa machozi.Amesema kuwa watu saba waliuawa.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa maafisa wa polisi walichukua hatua hiyo baada ya waandamanaji kuanza kuelekea katika makaazi ya bwana Shariif huku wakijaribu kuondoa vizuizi vilivyowekwa na polisi.
Amesema kuwa baadhi ya waandamanaji walifaulu kuingia katika jengo hilo.
Waziri wa Ulinzi amesema kuwa viongozi wa maandamano hayo wanajaribu kuchochea hali hiyo ili walaumu serikali kwa mauaji.
Amesema kuwa serikali itatumia nguvu kiasi kuwadhibiti waandamanaji hao.
|
0 Comments