Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova.
Na Mwandishi wetu
Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limesema kuwa limefanikiwa kukamata kundi la watu saba wanaotengeneza noti bandia za Dolla milioni moja na sitini na nne ambazo ni sawa na sh bilioni moja milioni mia saba na mbili na laki nne.
Kamanda Kova alisema tukio hilo lilitokea mnamo Agosti 4 huko Sinza katika Hotel iitwayo Mombasa Kinondoni.
Kova alisema polisi walipata taarifa toka kwa wasamaria wema na kuweka mtego wa kuwakamata ndipo askari walipofika eneo hilo na kukuta noti hizo zikiwa zimefungwa mabunda themanini na kasiki ndogo ambayo imefungwa kwa namba za siri.
Kova aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Ahmads Mohamed (50), mkazi wa Mombasa ambaye ni mfanyabiashara, Ichards Magoti (61), mkazi wa Musoma, Simoni Lukiko (58)mkazi wa Magomeni Kagera na Humprey leonard (34) mkazi wa Mburahati na wenzao watatu.
Katika tukio jingine, Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, limefanikiwa kukamata Bunduki aina ya SMG ikiwa na risasi 151 na magazine 2.
Kova alisema tukio hilo lilitokea wakati wa oparesheni ya kuhakikisha usalama katika jiji la Dar es salaam kwa muda wa wiki 2.
Aliongeza kuwa katika tukio hilo Jeshi la polisi limefanikiwa kukamata majambazi sugu 18 wakiwa wamejipanga kufanya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
|
0 Comments