Wakuu wa kandanda wa Sierra Leone wanasema mechi ijayo ya duru za mwanzo za Kombe la Afrika, baina ya Sierra Leone na Ivory Coast, itafanywa ingawa kuna ugonjwa wa ebola Afrika Magharibi.Shirika la Kandanda la Sierra Leone limesema itataja timu yao ambayo itakuwa na wachezaji walioko nje ya nchi.Ivory Coast imesisitiza kuwa haitaruhusu mechi hiyo kufanywa katika mji mkuu, Abidjan, kwa sababu ya wasiwasi wa kutapakaza virusi vya ebola.
Lakini haikutangaza wapi mechi itafanywa na pengine inaweza kupoteza mechi hiyo.
Huku nyuma nchini Nigeria, mjane wa daktari aliyekuwa mtu wa sita kufa kwa sababu ya ebola nchini humo, naye ameonekana ameambukizwa virusi.
Na wagonjwa watatu wa daktari huyo mjini Port Harcourt wamepelekwa katika zahanati maalumu lakini haikuthibitishwa iwapo kweli wana virusi vya ebola.
0 Comments