Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemfuta kazi waziri mkuu na mwandani wake Amama Mbabazi.
Kwenye taarifa yake Museveni alimshukuru bwana Mbabazi kwa mchango wake kwa nchi ya Uganda ambapo pia alimtangaza mrithi wake Ruhakana Rugunda ambaye sasa anasubiri kuidhinishwa na bunge.
Rais Museveni ametangaza kuwa amemteua daktari Ruhakaan Rugunda kama waziri mkuu mpya ambaye ataaanza kushikilia wadhifa wake mara moja.
Waziri mkuu anayeondoka Amama Mbabazi alionekana kuwa angemrithi rais Museveni lakini miaka mitatu ambayo amehudumu katika wadhifa huo uhusiano kati yake na Museveni haujakuwa mzuri.
Mapema mwaka huu chama kinachotawala kiliidhinisha azimio kikisema kuwa rais Museveni ambaye amekuwa uongozini kwa muda wa miaka 28 atakuwa mgombea wa pekee kwenye uchaguzi wa mwaka 2016.
Hata hivyo mkewe Mbabazi ambaye pia ni afisa wa cheo cha juu chamani amesema kuwa mumewe ameonewa.
Waziri mkuu mpya ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya awali alikuwa amehudumu kama waziri wa afya.
0 Comments