Rais wa Soko la Almasi la Antwerpen Mhe. Stephane Fischler (katikati) akizungumza na Mabalozi wa Afrika wanaokaa Ubelgiji wa nchi zinazozalisha almasi. Soko la Almasi la Antwerpen kila mwaka linauza almasi yenye thamani ya Euro bilioni 52. Rais huyo pamoja na mambo mengine amewaeleza Mabalozi mpango wa soko hilo kuanzisha utaratibu wa kutoa takwimu za uzalishaji na mwenendo wa bei ya almasi katika soko la dunia. Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala ameshiriki katika kikao hicho kilichofanyika Antwerpen Ubelgiji. |
0 Comments