Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
LEO ni siku ya kuzaliwa kwa Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alizaliwa tarehe 7 Oktoba, 1950 KIJIJI cha Msoga kilichopo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani katika iliyokuwa inaitwa Tanganyika. Alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Msoga kati ya mwaka 1958 na 1961.
Baada ya hapo alihamia shule ya kati(MIDDLE school) Lugoba kati ya mwaka 1962 mpaka 1965. Baada ya hapo akajiunga na shule ya sekondari Kibaha kwa ajili ya O’level.
Hiyo ilikuwa ni kati ya mwaka 1966 mpaka 1969. Baada ya hapo akaelekea shule ya sekondari Tanga kwa ajili ya A’Level. Mwaka 1972 mpaka 1975 alikuwa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam akisomea Uchumi.
|
0 Comments