Mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja kiongozi mwanzilishi wa bendi maarufu Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni ya kule Ujerumani,juzi kati Kamanda Ras Makunja aliwekwa kiti moto au kigoda cha moto na kituo cha TV cha Offener Channel ya Ujerumani. mwengozaji wa kipindi katika mahojiano hayo Bw.Fischer alimkutanisha Kamanda Ras Makunja na wataalam na wadau wa muziki wa kimataifa.
Akikaribishwa katika kipindi hicho mwanamuziki Ras Makunja ametajwa kuwa jamii ya ujerumani inauthamini na kuukubali mchango mchango wake wa kutumia muziki katika
kutokomeza ubaguzi,historia imemtaja Kamanda Ras Makunja na kikosi kazi Ngoma Africa band kuwa kuanzia mwaka 1993 alikubali kuzunguka ujerumani nzima kufanya maonyesho ya "WE ARE ONE" onyesho liliofanikiwa kuwaunganisha wageni na wenyeji
kazi ambayo haikuwa rahisi lakini ilifanikiwa.
Lakini pia wadau wa muziki na mtangazaji walitaka kujua inakuaje ? kwa muda wa miaka 21 Ngoma Africa band inadumu na kuendelea kuwanasa washabiki kwa wingi ??
Kamanda Ras Makunja akijibu swali hilo japokuwa alionekana si wakutaka kuweka hadharani kila mbinu,lakini alifunguka kwa kusema kuwa muziki unachezeka lakini pamoja na kuchezeka pia wanamuziki wa bendi ya Ngoma Africa band ni watumishi wa washabiki na wadau wa muziki kwa maana hii bendi inamilikiwa na washabiki na wadau ambao wao ndio wanayoitangaza. Sisi tuna vyombo vya muziki tu.Mimi naongoza bendi tu lakini wamiliki ni washabiki na wapenzi wa Ngoma Africa band , bandi hii ni sauti ya umma wa kimataifa pia ni sauti ya wasio sikika "Voice of speachless" ambayo inasikika kimataifa Ras Makunja alisema.
RAS MAKUNJA ALIPOITUMIA FURSA KWA KUWAOMBA MAPOROMOTA KUWAPA NAFASI WASANII WA TANZANIA !! walio nyumbani
Kama kawaida yake Kamanda Ras Makunja bila kujisihau wapi anatoka yaani mtanzania aliyekunywa maji ya bendera! alipoulizwa juu ya vipaji vya wafrika?
Kamanda Ras Makunja moja kwa moja aliwaomba wadau na maporomota wa kimataifa
kuwapa nafasi kubwa wanasanii waliopo nyumbani Tanzania kuja kushiriki maonyesho ya kimataifa, Ras Makunja aliwaomba na kuwashawishi maporomota na wadau hao
kuwa nchi ya Tanzania ina utajiri wa maelfu ya wasanii wenye vipaji vya ajabu wakiwemo wanamuziki,watengenezaji wasanaa za mikono wanawake kwa wanaume,wacheza maigizo,sarakasi,wachoraji,
Ninawaombeni nendeni Tanzania na mkitaka msaada wangu wa kuwaelekeza mimi nipo Tayari - Kamanda Ras Makunja alimalizia kwa kuwaomba wadau na maporomota.
Kamanda huyu wa Ngoma Africa Band Ras Makunja alionekana kutumia fulsa kwa
kuwapigania wasanii wa nyumbani ili wapate nafasi zaidi ya kimataifa.
Nje ya uringo alipoulizwa mbona ameifagilia Tanzania sana na swali lilikuwa wasanii wa Afrika, Makunja alijibu kwa mkato heti hata Umoja wa mataifa kila nchi ina balozi wake na akatimua zake.
burudika nao at www.ngoma-africa.com
wape shavu at www.facebook.com/
|
0 Comments