Kikundi cha The WT cha jijini Dar es Salaam kilichoshinda nafasi ya pili katika fainali ya shindano la Dance 100% 2014 likionesha umahiri wao wa kudansi katika fainali hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam.Ambapo kundi la”WAKALI SISI”toka kiwalani jijini liliibuka na ushindi huo na kujinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5 toka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania.

Meneja Uhusiano wa Umma  wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) akitaniana na kiongozi wa kundi la”Wakali sisi”la kiwalani jijini Dar es Salaam,Baraka Kambona(kushoto)alipokuwa akikabidhi hundi yenye thamani ya Tsh Milioni 5 kwa kundi hilo kama wadhamini wakuu wa shindano la Dance 100% kundi hilo liliibuka washindi katika fainali  ya shindano hilo. 

Washindi wa shindano la Dance 100% 2014 kundi la wakali sisi wakiwa kwenye picha ya pamoja na majaji wa shindano hilo na Ofisa matukio  wa Basata Kurwijira Magesa (kushoto)pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(wapili toka kulia)mara baada ya kutangazwa washindi wa shindano hilo na kujinyakulia kombe pamoja na kitita cha shilingi milioni 5 toka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania.

Washiriki wa shindano la dance 100% wa kundi la ”The Winners Crew” la jijini Dar es Salaam,wakionesha umahiri wao wa kudansi wakati wa mchuano wa fainali wa shindano hilolililoandaliwa na EATV lililofanyika  kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam.