Raia wa Brazil wanapiga kura kumchagua rais na viongozi muhimu wa majimbo ya taifa hilo kubwa lililopo Marekani kusini.
Wanawake wawili wanaonekana kushindana vikali katika kuwania wadhfa huo wa urais.
Rais Dilma Roussef- ambaye anaomba kuongeza kipindi cha miaka mingine minne ya kutawala anatarajia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa waziri wa zamani wa zazingira, mwenye siasa za ujamaa, Marina Silva.
Mgombea wa mrengo wa kati, Aecio Neves amekuwa akigawanya kura zao katika kura za awali za maoni.
Mwandishi wa BBC nchini Brazil anasema hali iliyopo sasa ni wazi kutakuwa na duru ya pili ya kura ya urais kati ya wanawake hao wawili.
Wapiga kura wanatarajia kuwachagua magavana wa majimbo na wabunge wa serikali kuu.
Matokeo yanatarajiwa kutangazwa punde tu baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika..
|
0 Comments