Aliyekuwa rais wa Madagascar Marc Ravalomanana amekamatwa muda mfupi baada ya yeye kurejea nyumbani baada ya kuishi uhamishoni kwa muda wa miaka mitano
Mwandhi wa bbc mjini Antananarivo amesema kuwa vitoa machozi vilirushwa na badaye vikosi vya usalama vikaonekana nje ya nyumba yake.
Serikali ya kisiwa hicho cha bahari Hindi mara nyingi imezuia kurudi kwake nyumbani tangu mpinzani wake Andry Rajoeline amuondoe madarakani kwa njia ya kijeshi.
Miaka minne iliyopita rais huyo wa zamani alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani bila ya yeye kuwepo mahakani kutokana na mauaji ya watu 30 wafuasi wa upinzani.
|
0 Comments