Uingereza inapeleka askari 750 kwenda Sierra Leone kusaidia kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola, anathibitisha waziri wa mambo ya nje Philip Hammond .
Uingereza pia itatuma meli yenye shehena ya dawa na helikopta tatu. Askari watasafiri wiki ijayo.
Hatua hii inakuja wakati waziri wa afya Jeremy Hunt anasema "kwa sasa inawezekana kwamba mtu mwenye Ebola anaweza kuingia Uingereza kwa njia moja au nyingine."
Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa watu 3,879 wamekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola Afrika magharibi.
Idadi kubwa ya vifo vimetokea Guinea, Liberia na Sierra Leone, ambako watu 879 wamekufa.
Hakuna tiba wala chanjo ya ugonjwa wa Ebola, ambao umeambukiza watu zaidi ya 8,000 katika maeneo yaliyoathirika zaidi na ugonjwa huo.
|
0 Comments