Wazazi wa Abdul-Rahman Kassig raia wa Marekani aliyekuwa akifanya kazi katika mashirika ya misaada ya kibinadamu nchini Syria ,wametoa rambi rambi zao kwa mtoto wao aliyeuawa kwa kuchinjwa na wapiganaji wa IS.
Wamesema kuwa wamejifunza kutokana na maujaji hayo na kwamba wamewasamehe wauaji hao japo kuwa awali mioyo yao ilikuwa na huzuni mkubwa na uchungu kufuatia tukio hilo.

Ed na Paula Kassig wadogo zake na Abdul Rahman Kassig wamemuelezea ndugu yao kwamba alikuwa mkweli na mfanyakazi mwaminifu katika mashirika ya kutoa misaada ya kibidamu ambaye alikuwa na mtazamo wa kutoa msaada na kujiepusha na udanganyifu wa aina yoyote.
Hata hivyo familia hiyo ya Kassig imetoa rai ya kufanyika kwa maombi maalumu kwa watu wa Syria nchini Iraq na duniani kote mahala ambapo watu wanakabiliwa na vitendo vya ukiukwaji wa haki.
Awali waziri wa kigeni wa Ufaransa Bernard Cazeneuve amesema kuna uwezekano mkubwa raia wa nchi hiyo walishiriki katika kitendo cha kumchinja Abdul kutokana na picha za video zilizoonyeshwa jumapili ambapo anaonekana Kassig na wanajeshi wengine 18 wa Syria.