Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikishuka kutoka kwenye tanki la kuhifadhia maji ya Mradi wa Maji wa Ruhuiko Kanisani utakaohudumia zaidi ya wakazi 3000 wa kitongoji ya Kijiji cha Ruhuiko Kanisani na maeneo ya jirani.
 Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikishuhudia kazi ya utandazi wa mabomba ya maji ya Mradi wa Maji wa Ruhuiko Kanisani. Hadi kukamilika kwake mradi huo utatumia zaidi ya shilingi milioni 480.
Msanifu wa Mradi wa Maji wa Ruhuiko Kanisani Bw. Elezear Ndunguru (Kulia) akitoa maelekezo kuhusu maendeleo ya mradi huo. Mradi huu unafadhiliwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia na unagharimu zaidi ya shilingi milioni 480 za Kitanzania. 
 Kiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Mwenye koti jekundu) akihoji masuala mbalimbali kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji kwenye manispaa ya Songea.
Msanifu wa Mradi wa Maji wa Ruhuiko Kanisani Bw. Elezear Ndunguru (Kulia) akisisitiza jambo wakati akizungumza na kiongozi wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri (Kushoto). Anayewasikiliza ni Mratibu wa zoezi hilo Bw. Senya Tuni.