Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula aliyekwenda kumjulia hali katika hospitali ya John Hopkins iliyopo Baltimore, Maryland, nchini Marekani, jana Jumapili, siku moja baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume. 

Rais Kikwete anaendelea vyema na alianza mazoezi ya kutembea, kuashiria kwamba mambo yote yanakwenda vizuri.Tuzidi kumuombea apate nafuu haraka ili arejee nyumbani kulijenga Taifa.