Rais wa Afrika ya Kusini bwana Jacob Zuma
Upinzani nchini Afrika Kusini unatarajiwa kuwasilisha bungeni hoja ya kutaka kumuondoa madarakani rais wa nchi hiyo.
Wabunge wa upinzani nchini humo wamesema kauli mbiu yao ni Rais Zuma lazima aende.
Wakati hayo yakijiri, Kamati ya wabunge wa chama tawala cha ANC watakuwa wakiwasilisha mbele ya Spika wa bunge uchunguzi wao walioufanya kuonyesha kuwa Rais Jacob Zuma hakuhusika na ubadhirifu wa kiasi cha dola millioni 22 zilizotumika kujenga Kasri lake huko Nkandla.