Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Nishati Duniani Bwana Selim Kuneralp (kushoto) na Mhandisi John F. Kitonga wa kitengo cha Maendeleo ya Nishati Wizara ya Nishati na Madini Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bwana Kuneralp amefika ofisi za Ubalozi wa Tanzania Ubeligiji kubadilishana mawazo na Balozi Kamala kuhusu kazi za Baraza la Nishati Duniani na jinsi Tanzania inavyoweza kunufaika na shughuli za Baraza hilo.