Diamond Platnumz akilakiwa na umati wa watu waliwafika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere akiporejea akitokea Afrika ya kusini ambao alitwaa tuzo tatu kwa mpigo
Msanii Diamond akionyesha Tuzo zake kwa mashabiki na wapenzi waliofika uwanja wa ndege kumpokea msanii huyoo.

MWANAMUZIKI Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' ametua nchini leo akitokea Afrika Kusini alipokwenda kushiriki zoezi la utoaji tuzo za Channel O ambapo alijinyakulia tuzo tatu kwa mpigo. Tuzo alizonyakua staa huyo ni pamoja na Most Gifted New Comer, Most Gifted Afropop na Most Gifted East kupitia wimbo wake wa Number One.