Manowari ya Marekani
Wanamaji kutoka Marekani wamesema kuwa wanapeleka moja ya Manowari ya kivita kutafuta ndege ya AirAsia iliyopotea tangu jumapili katika Bahari za Indonesia.
Manowari hiyo ijulikanayo kwa jina la USS Sampson inatarajiwa kufika leo katika bahari ya Java ikiwa ni siku ya tatu tangua kuanza msako dhidi ya ndege hiyo. Idadi ya wataalamu wa kimataifa wanaoitafuta ndege hiyo imeongezeka kwa sasa nchi za Singapore, Malaysia ,Australia,Korea Kusini,Thailand na China wanashiriki katika kazi hiyo.
Mkuu wa Operesheni ya uokozi na utafutaji ndege hiyo, Henry Bambang Soelistyo amesema kwa sasa kuna jumla ya Meli 30,ndege 15 na Helkopita kadhaa katika eneo la tukio.
ikumbukwe kwamba ndege hiyo ilipotea wakati ikisafiri kutoka Surabaya Indonesia kuelekea Singapore ikiwa na abiria 162.