Stori: Gladness Mallya/Ijumaa Wikienda
Mambo ya fedha! Takribani wiki saba tangu anyakue zaidi ya Sh. Milioni 500 baada ya kuibuka mshindi kwenye Shindano la Big Brother Africa ‘Hotshots’ 2014, Idris Sultan anadaiwa kubakiza takribani kiasi cha Sh. milioni 200 baada ya kudaiwa kununua mjengo wa ghorofa wenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 300.
Kwa mujibu wa Idris, nyumba hiyo ipo maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar hivyo kwa sasa naye ni baba mwenye nyumba.

Mjengo wa ghorofa uliononuliwa na mshindi kwenye Shindano la Big Brother Africa ‘Hotshots’ 2014, Idris Sultan.
Jamaa huyo alitarajia kuhamia kwenye mjengo huo jana Jumapili.
Mjengo huo una vyumba kadhaa, sebule mbili, bustani na eneo la kutosha la maegesho ya magari.
Habari zinadai kwamba kama kweli ametumia kiasi hicho cha fedha huku akimshukuru mtu aliyemtaja kwa jina la Mohamed kwa kufanikisha jambo hilo, basi atakuwa amebakizi milioni 200 ambazo wataalam wa mambo ya uchumi wanamshauri kufungulia kampuni au biashara.
Idris Sultan akipozi mbele ya mali zake.
Wataalam hao walifafanua kwamba, Idris anatakiwa kuzitumia fedha hizo kujiongezea kipato la sivyo atazitumia kuhudumia nyumba hiyo kwa vitu kama kulipia bili mbalimbali, kodi na kuajiri wahudumu.
“Anaweza akaona kwamba kununua nyumba ni matumizi mazuri ya fedha alizoshinda lakini anatakiwa awe makini, aidha kwa kufanyia biashara au kutoa huduma itakayokuwa ikimwingiza kipato.
“Pia asisikilize watu wanasema nini juu ya fedha zake. Anatakiwa kutimiza ndoto zake alizokuwa nazo kabla hajazipata,” alisema mmoja wa wataalam hao ambaye hakupenda jina lake liandikwe.