Prof. Mwandosya, (wa pili mbele) ,na ujumbe wake, wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Ashraf Mustafa,kuhusu usimamizi,udhibiti,na uendeshaji wa mitambo ya kuzalisha umeme.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya ( wa sita toka kushoto) na ujumbe wake wakiwa na Uongozi wa Bwawa la Umeme la Merowe wakiwa mbele ya Kitoleo cha Maji(Spillway) Wengine kutoka kushoto ni: Ngusa Izengo,Katibu wa Waziri;David Mziray kutoka Sumatra;Grace Nsanya;kutoka Wizara ya Maji;Wallace Chiwawa,TCAA;Hassan Amin Mohammed Ahmed Omer,Mkurugenzi wa Usalama wa Bwawa;Ashraf Mustafa,Meneja wa Uendeshaji;Mahgoub Eisa Khalil,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Umeme,Merowe;Felix Ngamlagosi,Mkurugenzi Mkuu,EWURA;Mhandisi Mustafa Hussein,Afisa Mwandamizi,Wizara ya Maji na Umeme,Sudan;Meneja wa Kituo; na Clemence Kichao kutoka TCRA. Prof.Mwandosya alipata nafasi ya kuongea na Waandishi wa Habari wa Sudan walioongozana na ujumbe wake huko Merowe,Sudan,akiwa mbele ya moja ya Piramidi za Merowe.Piramidi za Merowe zilijengwa zaidi ya miaka 7000 Kabla ya Ukristo,na ni zamani zaidi kuliko zile za Misri.
0 Comments