Hali ya sintofahamu ikiwa imetanda katika eneo la tukio baada ya shambulio hilo.
POLISI mmoja wa kike ameuawa kwa risasi huku wafagiaji wa mitaani wakijeruhiwa baada ya kushambuliwa na mtu aliyekuwa na silaha katika shambulio la pili ndani ya saa 24 lililotokea eneo la Montrouge jijini Paris nchini Ufaransa.

Shambulio la leo limetokea kusini mwa mji wa Paris huku mshambuliaji aliyekuwa amaevaa nguo ya kuzuia risasi 'bullet prof' akitumia silaha aina ya M5.
Polisi huyo alisimaa mtaani kukagua ajali iliyotokea barabarani kabla ya kushambuliwa na mtu huyo.
Shuhuda wa shambulio hilo anadai kusikia milio ya risasi tano kwenye tukio hilo.

Shambulio hilo limetokea ndani ya saa 24 baada ya shambulio la jana katika ofisi za magazeti ya vikatuni ya Charlie Hebdo jijini Paris, Ufaransa lililoua watu 12 na kujeruhi kadhaa. Bado haijafahamika kama shambulio la leo lina uhusiano wowote na lile la jana.

Eneo la Montrouge jijini Paris nchini Ufaransa lilipotokea shambulio la leo.

Mmoja wa majeruhi wa shambulio la leo akipatiwa huduma ya kwanza na kikosi cha uokoaji.