Rais Obama
Marekani inasema kuwa itafungua ubalozi wake nchini Cuba kuanzia mwezi Aprili.
Baada ya duru ya pili ya mazungumzo mjini Washington yenye lengo la kurejesha uhusiano kati yao mwanadiplomasia wa cheo cha juu wa Marekani katika nchi za Marekani ya kusini Roberta Jacobson, alisema kuwa itawezekana kufunguliwa kwa ubalozi kabla ya mkutano wa kimaeneo ambao utafanyika nchini Panama kuanzia tarehe kumi mwezi Aprili.

Mkuu wa ujumbe wa Cuba Josefina Vidal alisisitiza kuwa Marekani ni lazima iondoe Cuba kutoka kwa orodha ya nchi ambazo zinaunga mkono Ugaidi kabla ya kurejesha tena uhusiano huo.
Mwezi Disemba Cuba na Marekani walitangaza kuwa walikubaliana kuboresha uhusiano wao baada ya zaidi ya miaka 50 .