Katibu Mtendaji wa Iclusive Development Promoters& Consultants (IDPC) Kaganzi Rutachwamagyo (kulia) mwenyekiti SHIVYAWATA, Amoni Mpanju na  Mwenyekiti umoja wa watu wenye ulemavu, Zanzibar Ali Makame.Mtoa mada kaganzi akichokoza mada.
Wawakilishi mbalimbali wa vyama vya siasa wakichangia mada.Baadhi ya wadau na wanahabari.
Wadau mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja.

Makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu kwa kushirikiana na wanasiasa leo wamefanya mkutano mahsusi  kuhusu haki ya ushiriki wa watu wenye ulemavu  katika kura ya maoni na Uchaguzi Mkuu Tanzania  mwaka 2015.
Mkutano huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Blue Pearl Hotel uliopo Ubungo, jijini Da r es Salaam na kuhudhuriwa na walemavu wa ngozi (Albino) watu wasioona, walio na ulemavu wa viungo na wengineo.
Akizungumza katika mkutano huo, mwasilishaji wa  mada  Katibu mtendaji wa Inclusive Development Promoters& Consultants(IDPC) Kaganzi Rutachwamagyo amesema wanasiasa wanapaswa kutengeneza mazingira rafiki kwa walemavu ili waweze kushiriki katika kura ya maoni na uchaguzi mkuu, mwaka 2015 kwani ni haki yao kisheria,
Aidha Kaganzi amewataka  kudumisha amani katika kampeni za uchaguzi mkuu ili kuwavutia  walemavu kuhudhuria, kwani mara nyingi wanashindwa kuhudhuria kwa sababu mazingira si rafiki kwao.
“nawashauri wagombea urais kutokuwa na wakalimani wa lugha ya ishara ili kuwawezesha walemavu kuweze kujua kile kinachoendelea katika mikutano ya hadhara, televisheni na kadhalika.”
(HABARI/PICHA: GABRIEL NG’OSHA/GPL)