Bondia Mohamed Matumla kesho Machi 27 atapanda ulingoni kuzichapa kuwania ubingwa wa dunia wa WBF dhidi ya Wang Xin Hua raia wa China. Pambano hilo la raundi 12 la uzani wa Bantam limepangwa kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Katika pambano hilo mabondia Mada Maugo na Japhet Kaseba watapigana katika mpambano wa utangulizi wakifuatiwa na Kalama Nyilawila ambaye atapambana na Thomas Mashali na wengineo.
Mabondia wote hao leo wamepima uzito na afya zao kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari ‘Maelezo’. Angalia picha
0 Comments