Hii ni moja ya siri ya upendo wetu,mke anapofuata taratibu zote za mapenzi huwezi kuona penzi linayumba.Nampenda sana mama watoto wangu kama anavyonipenda
Mkiwa na upendo wa kweli amani haipotei,na mkiwa na ushirikiano wa kweli basi mtafurahia ndoa yenu kila kukicha,tunawashauri na wenzetu kupendana,kuaminia na kushirikiana kwa hali na mali ili kudumisha mapenzi yenu.
Mwisho kabisa niwatakie heri watu wote wenye ndoa changa ili nao waje kukomaa kama mimi na mke wangu na wale wenye ukomavu kama wetu kwenye ndoa nawaombea heri nao ili waendelee kudumu katika ndoa zao.
Leo hakutakuwa na habari yoyote mtandaoni kwani ni siku maalumu ya kusheherekea sikukuu hii mimi na familia yangu.siku njema wapendwa.
Maganga One.
1 Comments
wadau
FFU-Ughaibuni