Rais wa Sierra Leone Ernest Koroma kushoto na makamu wake Sam Sumana Kulia
Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma amemfuta kazi makamu wa rais kwa kutafuta hifadhi katika ubalozi wa kigeni nchini humo.
Siku ya jumamosi ,Samuel Sam Sumana amesema kuwa alimtaka balozi wa Marekani kumpatia hifadhi ndani ya ubalozi wa Marekani nchini humo akihofia maisha yake.

Awali wanajeshi waliizunguka nyumbani yake na kumpokonya silaha mlinzi wake .
Kumekuwa na wasiwasi kati ya rais na bwana Sam Sumana.
Hivi majuzi aliondolewa katika chama tawala cha All People Congress kwa udanganyifu na kuchochea ghasia.
Hatahivyo amekana madai hayo.