Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Kapteni Komba anatarajiwa kuzikwa kijijini Kwake Litui wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimfariji mjane wa marehemu Salome Komba katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro)

 Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal na wake zake Mama Asha na Mama Zakhia wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
  Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassa Mwinyi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.