Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo [jana]Machi 6, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Mkurugenzi wa Azam TV Bw. Dunstan Tido Mhando wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo[jana] Machi 6, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitangaza rasmi kuzinduliwa kwa studio mpya za stesheni ya Azam TV Tabata Relini jijini Dar es salaam leo[jana] Machi 6, 2015. Pamoja naye kwenye kilinge cha utangazaji ni mmiliki wa stesheni hiyo Bw. Saidi Salim Bakhressa.