Mmoja wa wanajeshi wa Ufaransa
Waendesha mashtaka nchini Ufaransa wanachunguza tuhuma za ngono kwa watoto zinazodaiwa kufanywa na wanajeshi wa nchi hiyo pindi walipokuwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Wizara ya Ulinzi imesema itahitaji kutolewa kwa adhabu kali zaidi dhidi ya yeyote atakae patikana na hatia.
Mashtaka hayo yamefunguliwa baada ya kupatikana kwa nyaraka zilizotolewa mwezi July na mfanyakazi mwandamizi wa Umoja wa Mataifa.
Afisa huyo alisimamishwa kazi baada ya kupewa nyaraka hizo za siri kwa Ufaransa. Farhan Haq, msemaji msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon, amesema Umoja wa Mataifa umefanya uchunguzi wa tuhuma hizo, ambazo itazifuatilia kwa kina.