Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao Shalua (kulia)akipokea tuzo aliyoipata Nalimi Mayunga mara baada ya kuibuka  mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Afrika.  Shughuli hii imefanyika jana katika halfa ya kumpongeza  Mayunga kwa kuiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars iliyofanyika  katika ofisi za BASATA. Akishuhudia  kushoto ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando
Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao Shalua (Katikati) akiongea katika halfa ya kumpongeza mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Airtel Trace Music Stars Afrika kwa kuibuka mshindi wa mashindano hayo na kuiwakilisha vyema Tanzania . halfa hiyo ilifanyika katika ofisi za BASATA Ilala Dar es Saalam. kushoto ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando


Baraza la sanaa Tanzania BASATA leo limempongeza mwakiliwa wa Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace kufatia ushindi alioupata katika mashindano ya muziki yaliyoshirikisha washiriki 13 toka nchi za Afrika .
Mwisho mwa mwezi wa tatu BASATA ilimkabidh bendera Mayunga na kumpa kibali cha kwenda kushiriki mashindano hayo yaliyokuwa yanafanyika nchini Kenya  na kumtakia kila  laheri katika mashindano hayo ambapo mwakilishi huyu aliweza kufanya vizuri na kuibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Star wa Afrika
Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao Shalua katika halfa fupi ya pongezi kwa Nalimi Mayunga katika ofisi za BASATA alisema”  Ushindi huu ni  furaha kubwa kwetu sisi Baraza la Sanaa la Tanzania kwani tunayo dhamana ya kuhakikisha tunaendeleza sanaa nchini  kwa tunashirikiana na wadau mbalimbali nchini katika kuwawezesha   vijana wenye vipaji kukuza sanaa zao ndani na nje ya nchi.
Nachukua fulsa hii kwa niaba ya BASATA kumpongeza Mwakilishi wetu Nalimi Mayunga kwa kufanya vizuri na kushinda mashindano haya. 
Nawashukuru sana Airtel kwa kufata taratibu stahiki na kushirikisha BASATA tangu mashindano haya yaanze ikiwa ni kusajili  kampuni yao na kupata hati ya kufanya shughuli za sanaa na pia kutushirikisha katika mchakato mzima wa mashindano haya na kumleta mshindi huyu kuchukua hati maalumu ya kusafiri na kuagwa rasmi wakati wa kuondoka kwenda kwenye mashindano ya Afrika.  Kwakweli huu ni mfano wa kuigwa na wadau wengi na wasanii kwa ujumla, kufata taratibu na kupata vibali maalumu pindi wanapoenda nje ya nchi kufanya shughuli za sanaa na kuwakilsisha nchi yetu.
Natoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi pindi awamu ya msimu wa pili wa mashindano haya ya Airtel Trace yatakapotangazwa ili nao waweze kupata nafasi ya kushiriki na kuinua vipaji vyao. Aliongea Shalua
Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw Jackson Mmbando alisema  Tunawashukuru watanzania wote walioshiriki katika shindano hili  tangu tulipolizindua.  tunampongeza sana mayunga kwa ushindi huu. Nalimi Mayunga ameweza kujishindia dili la kwenda marekani na kupata mafunzo chini ya usimamizi wa Akon,na pia kuweza kurekodi wimbo na video yake ya kwanza vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya dola za kimarekai 500,000/= Tunategemea baada ya mafunzo hayo na kutoa wimbo wake na Akon basi mayunga ataendelea kufanya vizuri na hatimae kuweza kuzifikia ndoto zake.
Airtel ilimkabithi Mayunga zawadi ya shilingi million 50 za kitanzania kufatia ushindi wake hapa nchini  na sasa anajiandaa kwenda marekani na kufanya kazi na msaani nguli Akon.
Akiongelea ushindi wake Mayunga alisema, nawashukuru sana watanzania kwa kunipigia kura toka mashindano haya yaanze, najisikia furaha kupata nafasi hii ya pekee na naamini safari yangu nchini marekani itakuwa ya mafanikio makubwa na mwanzo wa mafanikio katika kuzifika ndoto zangu za kuwa mwanamuziki nyota ndani na nje ya nchi.
Nawashukuru Airtel  kwa kuanzisha mashindano haya na BASATA kwa kunipa ushirikiano wakati wote wa mashindano. Natoa wito kwa watanzania na vijana wenzangu kuchangamkia fulsa hii pindi msimu wa pili wa mashindano haya yatakapotangazwa na kuanza .
Mashindano ya Afrika yalimalizika  kwa mtanzania kushika nafasi ya kwanza , Nigeria nafasi ya pili  na Congo Brazavile nafasi ya tatu.