Vijana wa barza ya HATUDANGANYIKI ya Kiwengwa Cairo wakimsikiliza Maalim Seif wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika barza hiyo (Picha na OMKR)
Na Hassan Hamad, OMKR
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameweka mawe ya msingi na kupandisha bendera katika matawi na barza sita za CUF ndani ya Jimbo Kitope Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja.
Matawi na barza alizoweka mawe ya msingi ni pamoja na Kiombamvua, Mkaratini, Mgambo, Kilombero, Kipandoni na Kiwengwa Cairo.
Hata hivyo, mkutano wa hadhara uliokuwa ufanyike katika viwanja vya Kipandoni umehairishwa, kwa madai kuwa haukupata kibali kutoka kwa jeshi la polisi. |
0 Comments