MKUTANO WA UVCCM MJINI MOSHI UMEWAAMSHA WANANCHI
Kijana Daudi Mrindoko awambia wananchi wasikubali Kudanganywa tena!
Moshi,Kilimanjaro,
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mjini Moshi ulifanya mkutano wa hadhara siku ya jumamosi 25 April 2015 katika viwanja vya maduka Mpangano-Kiusa Moshi Mjini.katika mkutano huo mmoja wa waliozungumza jukwaani ni mjumbe
wa UVCCM mkoa Kilimanjaro Bw.Daudi Mrindoko aka Obama wa Moshi kama wanavyomuita wenyewe,Mrindoko alitumia muda mchache tu katika hotuba yake
alianza kwa kuuliza kwa kuamsha watu kwa swali " NIni walichokifanya Chadema hapa? Kipi cha maendeleo? Chadema wamewafanyieni nini? hapa Moshi? Chadema waje hapa watueleze? wasilete blah blah" kijana huyo Daudi Mrindoko akishangiliwa kwa mayoe CCM hoyeee! inaonyesha jinsi ananyorusha
dongo au kuwatia ugoro puani na kuwapigisha chafya wapinzani mjini Moshi,ambako siku za hivi karibuni kumekuwa na matukio ya wafuasi wa Chadema kujiunga CCM kwa kasi sana.
Mjumbe huyo wa UVCCM Bw.Daudi Mrindoko alimalizia hotuba yake kwa jiwe lingine la kusema"Mzee Akiwa Mwongo uzeeni Alivyokuwa mtoto alikuwaaje???"
akishangiliwa na wananchi CCM hoyee! CCM hoyeee!, na kuwasii watu wa Moshi mjini
wasikubali tena kudanganywa wala kukandwa kwa kufanyiwa masaji na mgongo wa chupa ,na wananchi wakiitikia kwa mayoe Uwongo sasa mwisho,CCM hoyee kijana Daudi Mrindoko anashuka jukwaani kwa kujiamini.wenyewe moshi wanasema
"Moshi kunafukuta Moto 2015"
|
0 Comments