"Mjini Moshi kunafuka moshi lazima chini kuna moto 2015"
WANANCHI WANAMSHAWISHI KIJANA DAUD MRINDOKO KUGOMBEA UBUNGE
Mamia ya wakazi wa Moshi mjini wamefunguka na kumshinikiza kwa kumshawishi kijana moja ajulukanae kwa jina la Daudi Mwidadi Mrindoko achukue fomu za kugombe ubunge wa jimbo hilo la Moshi mjini,mamia na kinamama na kina baba,vijana na wazee wa mji wa Moshi wanamtaja kijana Daudi Mrindoko kuwa
ndio tochi na dira ya itakayo waonyesha njia ya mafanikio zaidi 2015 alisema
mama moja Merry Kimaro kutoka kundi la wafanyibiashara wadogo Moshi sokoni.
Kijana mwingine aliyejitambulisha kwa jina Elias Mushi mwendesha boda boda
alijigamba kwa kusema kuwa heti Daudi Mrindoko ndio Obama wa mjini Moshi
kijana ambaye ni daraja kati ya jamii vijana kwa wazee,wanawake kwa wanaume,
Tulitaka kumjua zaidi huyu Kijana Daudi Mrindoko na kumtafuta ili kupata kauli yake
lakini juhudi ziligonga ukuta tuliambiwa amesafiri.
Mzee moja aliyejitambulisha kwa jina Gasper Temu mfanyi biashara alisema wazee wa Moshi wangependa sana kupata mbunge kijana ambaye ni rahisi kumtuma,kumshauri na kumkosoa unajua sisi wafanyi biashara na wakulima hapa
Moshi tunahitaji mabadiriko ya kasi kubwa ili tupate kusonga mbele alisema mzee
Gasper Temu.
"Mjini Moshi kunafuka moshi lazima chini kuna moto 2015"
|
0 Comments