Waziri wa nchi Ofisi ya Rais -Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya akifungua kisima cha maji cha Mradi wa SEMUSO uliopo Kibandamaiti, Zanzibar.Nyuma yake mwenye mawani ni Mheshimiwa Mussa Mussa Mbunge wa Amani.
Baada ya kufungulia bomba la maji ya Mradi wa SEMUSO,Kibandamaiti,Zanzibar,Waziri Mwandosya alimtwisha ndoo ya maji Ndugu Ali Magoha, Mjumbe wa Kamati ya Mradi wa SEMUSO, kuashiria kuyafikisha maji kwa watumiaji.
Tanki la maji la Mradi wa Maji wa SEMUSO lililo Kibandamaiti,Zanzibai,Mradi uliozinduliwa na Waziri Mwandosya.
0 Comments